Mzozo Wa Ardhi Ambao Umekuwa Ukikumba Shule Ya Msingi Ya Vikutsa Iliyoko Eneo Bunge La Shinyalu Kaunti Ya Kakamega Umefikia Kikomo Hii Ni Baada Ya Afisi Ya Hazina Ya NG-CDF Ya Eneo Hilo Kupeana Hundi Ya Shilingi Milioni 3.6 Kwa Shule Hiyo Kwa Minajili Ya Kununua Shamba La Shule
Akizungumza Baada Ya Kukabidhi Shule Hiyo Hundi Ya Pesa Ya Kununua Ardhi Ya Shule Hiyo, Mbunge Wa Eneo Hilo Fred Ikana Ameelezea Kujitolea Kwake Kuhakikisha Kwamba Shule Hiyo Inaendeshwa Bila Kuingiliwa Na Wanajamii
Amehidi Kushughulikia Suala Ya Ukosefu Wa Walimu Katika Shule Hiyo, Hii Ni Baada Ya Mwalimu Mkuu Wa Shule Hiyo Kudokeza Kuwa Shule Ya Vikutsa Ina Walimu Wanne Pekee Ambao Wameajiriwa Na Tume Ya Tsc Jambo Analosema Linaathiri Viwango Vya Elimu Katika Shule Hiyo
Hata Hivyo Ikana Alitumia Fursa Hiyo Kupigia Debe Serikali Ilioko Mamlakani Akifichua Kuwa Mikakati Imewekwa Ya Kuhakikisha Kwamba Barabara Za Eneo Hilo Zinakarabatiwa Na Wenyeji Kuunganishiwa Na Nguvu Za Umeme.
NA MARY OWANO-RIPOTA.
No Comments Yet...