Rais William Ruto,Kinara Wa ODM Raila Odinga Na Gavana Wa Nairobi Johnson Sakaja Wamefanya Mkutano Na Wawakilishi wadi Wa ODM Kulishawishi Bunge La Kaunti Hiyo Kutupilia Mbali Msukumo Wa Kuondolewa kwake Sakaja Madarakani.
Akihutubia Wanahabari Baada Ya Mashauri Hayo Ya Faragha, Mwenyekiti Wa ODM Nairobi George Aladwa Alisema madiwani Katika Chama Cha ODM Wamekubali Kutupilia Mbali Msukumo Wa Kumtimua madarakani Ili Kumpa Gavana Wa Nairobi Fursa Ya Kubadilisha Mtindo Wake Wa Uongozi Na Kurekebisha Makosa Yaliyoibuliwa Na Wawakilishi Wa Wadi.
Wawakilishi Wadi Walikuwa Wanapania Kuwasilisha Mswada Wa Kumtimua Sakaja Kwa Madai Ya Kuwatenga Kwenye Miradi Ya Maendeleo. Hata hivyo, Ruto Na Raila Wamempa Sakaja Siku Sitini Kutatua Mzozo uliopo.
NA DELVIS OLINGA.
No Comments Yet...